05 May 2013

TAARIFA za AWALI JUU YA BOMU....mmoja auawa,62 majeruhi

Hili ndilo kanisa iliyoshambuliwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono jijini Arusha

 MTU mmoja amefariki dunia na wengine 62 wamejeruhiwa vibaya katika shambulio la kigaidi iliyotokea leo asubuhi katika Kanisa la Katholiki Parokia ya Ola City Jijini Arusha.
Majeruhi wa tukio hilo wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ausha, Mount Meru
kwa matibabu zaidi, taarifa zilizo hivi sasa zinadai kwamba mtu mmoja anashikiriwa na Jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo.
Shambulio hilo la kigaidi limeacha maswali mengi bila majibu huku jeshi la Polisi Arusha likiendelea kumhoji mtuhumiwa huyo, shambulio hilo lilifanyika wakati wa uzinduzi wa kanisa hilo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname