Moja kati ya ajali ya basi la Taqwa (picha na maktaba yetu)
.......................................................
Abiria saba waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 273 CDR kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Malawi wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jioni jana katika eneo la Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
.......................................................
Abiria saba waliokuwa wakisafiri na basi la kampuni ya Taqwa lenye namba za usajili T 273 CDR kutoka jijini Dar es Salaam kwenda Malawi wamekufa papo hapo na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyotokea jioni jana katika eneo la Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.
mmoja
kati ya mashuhuda aliyejitambulisha kwa jina la Dkt Matatala alisema
kuwa ajali hiyo imetokea JANA mida ya saa 11 jioni wakati basi hilo
likitokea Dar es Salaam kwenda
nchini Malawi.
nchini Malawi.
Alisema
kuwa chanzo cha ajali hiyo ni lori lenye namba za usajili T 104 DZZ
ambalo lilikuwa likitokea Makambako kuelekea Iringa,lori lililokuwa
likijaribu kulipita lori lenye namba za usajili T 227 AVC na kushindwa
kupita na kuishia kugongana uso kwa uso na basi hilo ambalo pia lilikuwa
likija kwa mwendo wa kasi.
Kwa
mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo wamesema kuwa ajali hiyo imetokea
katikati ya mji wa Nyololo ambapo ni jirani kabisa na eneo lenye matuta
ya kuzuia magari kwenda kwa mwendo kasi.
Alisema
kuwa hadi majira ya saa 12.45 jioni maiti tano zilikuwa zimetolewa
katika basi hilo la Taqwa na kuwa jitihada za wasamaria wema kutoa maiti
na majeruhi katika eneo hilo zimeendelea kufanyika.
Mbali
ya maiti hizo pia alisema jumla ya majeruhi 20 waliokolewa na
kukimbizwa katika Hospitali ya wilaya ya Mufindi kwa matibabu zaidi. Dkt
Matatala alisema kuwa katika tukio hilo wananchi wameweza kuimarisha
ulinzi zaidi katika eneo hilo ikiwa ni pamoja na kulinda mali za
majeruhi na abiria waliopoteza maisha yao kwa ajili hiyo.
Wakati
huo huo wananchi wa eneo hilo la Nyololo wameelekeza lawama zao kwa
jeshi la polisi wilayani Mufindi kwa kuchelewa kufika katika eneo la
tukio na kuwa taarifa wamepewa mapema ila hadi majira ya saa 12.50
hakukuwepo na askari aliyefika eneo hilo.
Hii
ni ajali ya pili kutokea katika wilaya ya Mufindi kwa kipindi cha wiki
moja baada ya ajali nyingine mbaya kama hii kutokea eneo la Mafinga kwa
gari ndogo iliyokuwa ikiendeshwa na paroko wa kanisa katoliki Ifunda
marehemu Alfonce Mhamilawa kutokea kwa kuingia nyuma ya lori.
No comments:
Post a Comment