HII KAULI ALIYO ITOA MWENYEWE KUTOKANA NA TUKIO HILO
“kiukweli mimi kama Jacquline Wolper
sina ubaya na mtu yeyote, ila nmeshangaa kuona
watu nisiyo wajua kuja
usiku wa manane na kunichomea gari yangu. Kiukweli siwezi kumuhisi mtu
ila najua ni lazima atakua mtu asiependa maendeleo yangu ni ni mtu mbaya
sana kwangu. Na inawezekana kabisa alipanga kunia lakni kwa bahati
nzuri siku hiyo sikua nyumbani nilikua nimesafiri. Tukio lilitokea usiku
wa tarehe 23/10/2012 ambapo mtu alitumia matambara yaliyo na mafuta ya
taa au Petrol akiwa kwa nje ya ukuta wa nyumba yangu akiwa anarusha kwa
ndani. Nimepeleka taarifa kituo cha Polisi kawe kwa kutaka msaada wa
kiupelezi na nitakua nawapa taarifa za kila kinachoendelea. Namshukuru
Mwenyezi Mungu kwani niko salama”