Klabu ya bingwa ya Tanzania bara Simba Sports Club leo imetupa karata nyingine kwenye michuano ya Urafiki inayofanyika huko Zanzibar kwa kupepetena na washindi wa pili wa ligi kuu ya Vodacom msimu uliopita
klabu ya Azam.
Matokeo kwenye mchezo huo wa pili wa michunao hiyo yameishia kuwa sare ya 1-1. Simba ndio waliokuwa wa kwanza kufunga goli lilowekwa kimiani na mshambuliaji wake mpya Danny Mrwanda katika dakika ya 35, kabla ya Azama hawajasawazisha kupitia kwa mchezaji wao mpya kutoka Kenya George Odhiambo 'Blackberry' sekunde kadhaa kabla ya filimbi ya mapumziko kupulizwa.
Azam walicheza pungufu kwa takribani dakika 35 baada ya kiungo wao Abdulhalim Humud kupewa kadi nyekundu kwenye dakika ya 52.
Simba sasa inaongoza kwenye kundi lake kwa pointi nne, mabao matatu ya kufunga na mawili ya kufungwa, wakati Azam FC ni ya pili kwa pointi zake mbili.
chanzo-shafiidauda
No comments:
Post a Comment