Siku
chache baada ya mchezaji Shedrack Nsajigwa kumaliza mkataba wa
kuichezea klabu ya Yanga huku akiripotiwa kuwepo nchini Kenya akifanya
mazungumzo na klabu ya Gor Mahia, leo taarifa za uhakika kutoka kwenye
kamati ya usajili ya Simba, zinasema viongozi wa mabingwa wa Tanzania
wapo tayari kumsaini nahodha huyo wa zamani wa Yanga na Taifa Stars.
Simba
ambao leo hii wamepata pigo baada ya beki wao wa upande wa kulia Said
Nassoro Chollo kuripotiwa kupata majeraha makubwa kama yale yaliyompata
Uhuru Seleman, wanamuona Nsajigwa kama mbadala halisi atakayefaa kuziba
mapengo kwenye safu ya ulinzi ya timu hiyo.
Mtoa
taarifa anasema, "Nsajigwa bado ni mchezaji mzuri sana, na uwezo mkubwa
na kikubwa zaidi ni uzoefu alionao ambao ni hazina kubwa kwa klabu kama
yetu ambayo sasa tunajaribu kuingiza vijana wadogo kama akina Singano,
na ndio maana tumeamua kuanza harakati za kumsajili na kwa hakika
tutafanikiwa."
CHANZO -SHAFII BLOG
No comments:
Post a Comment