15 June 2012

Diamond Katishaaa...ONA KIASI CHA PESA CHA MKATABA ALIO SAINI DIAMOND KUPIGA SHOW MTWARA




Hapa chini ni mkataba ambao amelamba kutoka kampuni ya Emilates Hall kupiga shoo huko pande za Mtwara

Chini ni sehemu ya inayoonesha sahihi za wahusika wote:-

KUFUATIA mafanikio alinayoyapata hivi sasa kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya Bongo, staa wa muziki huo Naseeb Abdul ‘Diamond’ ndiye mkali aneingiza mkwanja mrefu zaidi kuliko nyota wote wanaotamba hivi sasa hapa nchini.

Uchunguzi uliofanywa na Mpekuzi umebaini kuwa Diamond anaingiza kiasi cha shilingi za kibongo Milioni 16 kwa kila shoo mbili anazofanya akiwa ndani na nje ya jiji la Bongo.
Katika kuhakikisha kuwa ukweli unapatikana mpekuzi ilimsaka Diamond na baada ya kufanikiwa kumpata alikiri kufikia kiwango hicho .

“Nashukuru Mungu kwa kufika hapa na ukweli ni kuwa nalipwa mkwanja huo na hii imekuja kufuatia kuweka nguvu zangu katika muziki na kufanya vitu vizuri kwa kuwa gemu ndiyo maisha yangu” alisema Diamond.
Akiendelea zaidi nyota huyo wa ‘Songi’ la ‘Mawazo’ alianika kuwa mafanikko haya yanakuja pia kutokana na sapoti anayoipata kutoka kwa watu wake wa karibu akiwemo Mama yake mzazi na wengine kibao.
chanzo-audiface blog

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname