Kocha
Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza
kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia
hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.
Akitangaza
kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu,
Kim amesema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi
anayocheza na ubora wake.
Wachezaji
walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na
Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo
(Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam),
Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na
Juma Nyoso (Simba).
Viungo
ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari
(Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward
Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu-
U20).
Washambuliaji
ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo),
Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi
(Simba) na John Bocco (Azam).
Stars
inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi
ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini
Abidjan.
No comments:
Post a Comment