Mario Balotelli nyota wa soka nchini Italia ambaye
pia ni mchezaji mweusi wa Klabu ya Manchester City ya Uingereza amesema
ataondoka uwanjani endapo atakejeliwa kutokana na rangi yake wakati wa
mchuano wa kombe la Mataifa Ulaya katika nchi za Poland na Ukraine mwezi
Juni.
Matamshi yake yanatokea kufuatia makala ya BBC
ambayo yaliangazia ghasia katika viwanja vya soka kutokana na ubaguzi wa
rangi katika nchi hizo mbili.Makala hayo yalionyesha mashabiki wakizungu wakiwakejeli wachezaji weusi na kuwashambulia mashabiki wenye asilia tofauti na kizungu.
Wanasiasa na maafisa wa soka kutoka nchi hizo wamesema tatizo hilo limetiwa chumvi.
Kukejeliwa kwa ubaguzi wa rangi dhidi ya Balotelli nchini Italia mwaka 2009 kulifanya shirika la soka Ulaya UEFA kuweka sheria ya kuwalazimisha marefa kusimamisha mechi ikiwa kejeli za ubaguzi wa rangi zitaendelea
No comments:
Post a Comment