21 April 2012

Breaking Newzzzzzz MAWAZIRI SABA WAJIUZURU

HATIMAYE mawaziri saba kati ya nane wakiwemo wanaokabiliwa na tuhuma za ubadhirifu, wamekubali kuandika barua za kujiuzulu wenyewe kwa kile kilichoelezwa kuwa ni kukinusuru Chama cha Mapinduzi (CCM).

Habari za kuaminika kutoka mjini Dodoma zimesema kuwa mawaziri hao, walilazimishwa kujiuzulu katika kikao cha dharura kilichokuwa chini ya uenyekiti wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilichofanyika mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge.

Taarifa zimewataja waliokubali kujiuzulu kuwa
ni pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami;
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika;
Waziri wa Uchukuzi Omari Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni:
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja;
Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya;
na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro Nyarandu.
Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye alishambuliwa vikali kwa kuitwa kinara wa ufujaji, hakuwepo katika kikao hicho kwa madai kuwa yuko nje ya nchi, anasubiriwa aungane na wenzake kuachia ngazi.
C HANZO MPEKUZI BLOG

2 comments:

  1. mafisadi hawa wache wajiuzuru..na huyo mkulo asizuge yupo nje aje abwage manyanga hapa hatutaki mbwembwe bila maendeleo

    ReplyDelete
  2. baada ya hapo mchakato wa kuwapeleka mahakamani pale kwenye ushahidi wa wazi uanze mara moja!

    ReplyDelete

Comments system

Disqus Shortname