01 November 2011

Miss Tanzania atinga 16 bora ya Beauty with Purpose


















Salha Israel amefanikiwa kuingia nusu fainali ya taji la
 Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) 
yaliyofanyika juzi nchini Uingereza.

Akizungumza kutoka London jana, Salha alisema kuwa
 katika taji hilo, mrembo huyo aliwasilisha kazi yake ya 
Jamii aliyoifanya kwenye hospitali ya Muhimbili ambako
 alisaidia watoto wenye matatizo ambao wanazaliwa chini
 ya mwezi moja.
Salha alisema kuwa katika shindano hilo, Salha aliwakilisha
 DVD inayonyesha jinsi gani alivyomsaidia mtoto aliyezaliwa 
kwenye hospitali hiyo huku akiwa na kidonda kikubwa mgongoni.
“Haikuwa kazi rahisi kwa majaji wa shindano hilo kuona 
ninavyofanya kazi ya kumsaidia mtoto huyo, ni kazi ambayo
 imewafanya waikubali
 kwani ipo katika majukumu ya Kamati ya Miss World
 mbali ya shindano lenyewe la urembo,” alisema Salha
 kwa njia ya simu.


Alisema kuwa amefarijika kuingia katika hatua hiyo ya 16 bora 
katika shindano hilo ambalo lilishirikisha jumla ya warembo 122
 kutoka nchi mbali mbali.
“Ninachokisubiri sasa ni fainali ya taji hili ambapo mshindi
 ataingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya
 mashindano hayo ambayo itashirikisha si chini ya warembo 20,” 
alisema.

Kuhusiana na mashindano, Salha alisema kuwa mashindano
 ni magumu ukilinganisha na mashindano ya Miss Tanzania
 kutokana na mambo makubwa moja.

Alisema kuwa sababu hiyo ni idadi ya washiriki ambao ni wengi
 ukilinganisha na warembo 30 wanaoshiriki Miss Tanzania na
 vile vile wapo bora zaidi kulinganisha na mashindano ya kitaifa.

“Ninawaomba Watanzania ni waniombee ili niweze kufanya
 vyema katika mashindano, ni magumu kwa kweli,” alisema.

Mkurugenzi wa Lino International Agency, Hashim "Uncle"
Lundenga alimpongeza Salha kwa hatua hiyo na kusema japo
 anakabiliwa na kibarua kikubwa ili aweze kufanya vyema.
"Ni matokeo mazuri, lakini kazi bado ni kubwa, tunatakiwa 
kumwombea ili aweze
kufanya vyema zaidi," alisema Lundenga.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname