Shirika
la
ndege la Etihad leo limekaribisha hukumu ya mahakama ya juu ya utawala
mjini Luneburg, Ujerumani ambapo mahakama imepinga hukumu ya awali na
hivyo
kuiruhusu Etihad kuendeleza safari zake 26 kati ya 31 za ‘makubaliano’
kati yake na Airberlin katika kipindi
cha baridi kinachoisha Machi 26, 2016.
“Tungependa
kuwatia moyo wateja wetu waliopo Ujerumani waendelee kuwaunga mkono Airberlin
na wafanyakazi wake 8,000 ambao kwa njia moja au nyingine wameathirika na
shambulio endelevu juu ya biashara yao”
Mahakama
ilikubali
kwamba ‘makubaliano’ 26 kati ya 31 yaliyopendekezwa ni halali kisheria
ukijumuisha na mengine 50 yaliyopitishwa na Airberlin, mapendekezo 76
kati ya 81 yamepitishwa
moja kwa moja, ikiwa ni asilimia 94 ya mapendekezo yaliyowasilishwa
awali.
Maamuzi
haya ya mahakama, juu ya makubaliano ya huduma za anga kati ya Umoja wa nchi za
Falme za Kiarabu na Ujerumani yanamaanisha kwamba shirika la Etihad
litaendelea na safari zake hata baada ya ratiba yake ya msimu wa
baridi
Rais
na Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Etihad, James Hogan, alisema: “Tumeridhishwa
na hukumu iliyotolewa na mahakama kuhalalisha asilimia 94 ya makubaliano. “Hukumu
hii ni ushindi kwa wateja na wapinzani wetu waliopo Ujerumani.
“Tunaendelea
kuungana na mshirika wetu, Airberlin, na tutaongeza juhudi zetu mara mbili ya
awali ili kuleta ushindani mbadala na mkubwa kwa shirika la ndege la Lufthansa, ambao kwa sasa ndio
wametawala sana anga za Ujerumani.’
No comments:
Post a Comment