Baraza la
Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya
kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi
wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani
hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.
Akitangaza
matokeo hayo jana Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo
Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika
kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango
cha ufaulu.
Jumla ya
wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87
waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D.
Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu
usioridhisha.
Aidha
wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia
89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi
waliofanya vibaya ili wawasaidie kuimarika na waweze kupata ufaulu mzuri
No comments:
Post a Comment