Michuano
ya gofu ya Waitara yanayodhaminiwa na Kampuni ya bia ya Serengeti kupitia pombe
yake kali ya Jonnie Walker imefana na kumalizika vizuri siku ya jumamosi ambapo
MCHEZAJI George Nyakundi ameibuka mshindi wa jumla wa mashindano ya kila mwaka
ya Kombe la Waitara yalilofanyika kwenye Viwanja vya gofu vya Klabu ya Jeshi la
Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo jijini Dar es Salaam.
Nyakundi
anayecheza katika kiwango cha ubora wa mchezo wa gofu (handicap) 22 alionesha
kiwango cha juu zaidi katika mashindano hayo kwa kupiga mikwaju nett 65 na kuwashinda
wachezaji zaidi ya 118 waliokuwa wakiwania Kombe hilo.
Nafasi
ya pili ya jumla ilikwenda kwa Michael Obare ambaye alichuana vikali na mshindi
akirejea na mikwaju nett 66.
Akizungumza
na waandishi wa habari waliofika katika viwanja hivyo, Meneja Chapa wa pombe
kali wa kampuni ya bia ya Serengeti Shomari Shija alisema kuwa wamedhamini
mashindano hayo kwa mara ya tano sasa ili kuendelea kuenzi heshima ya muasisi wa
klabu hiyo Jenerali Mstaafu George Waitara.
Akitangaza
matokeo ya washindi mbalimbali katika makundi tofauti Kapteni wa klabu ya gofu
Lugalo Japhet Masai alisema katika kundi la wachezaji wa viwango vya Daraja A
ambao ni wa kiwango cha juu katika mchezo huo mchezaji chipukizi Suleiman Kessy
mwenye handicap 9 alishinda kwa kupiga mikwaju nett 69, Jumanne Ally handicap 8
alishika nafasi ya pili akiwa na mikwaju 70, wakati Juma Likuli mwenye handicap
8 alimaliza nafasi ya tatu akiwa na mikwaju 70 pia.
Mchezaji
Nicolaus Chatanda handicap 11 alishinda kombe kwa wachezaji wa Daraja B akiwa
na mikwaju 68, akifuatiwa na nahodha wa Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam, Akhil
Yusufali handicap 16 akiwa na mikwaju 71 na Priscus Nyoni handicap 12 alishika
nafasi ya tatu akiwa na mikwaju 72.
Kelvin
Manuhwa handicap 19 alishinda kwa kundi la wachezaji wa Daraja C akiwa na
mikwaju 72 na kufuatiwa na R. Rwiguza handicap 24 aliyepiga 74.
Kundi
la wachezaji waandamizi wanaume kombe lilikwenda kwa Joseph Tairo handicap 13
mikwaju 73, nafasi ya pili alikuwa Jenerali Mstaafu Mirisho Sarakikya handicap
19 aliyepiga mikwaju 73 pia , wakati Edmund Mndolwa handicap 9 alipiga mikwaju
74 na kumaliza nafasi ya tatu.
Pricilla
Karobia handicap 17 alishinda kwa upande wa wachezaji wakongwe wanawake akiwa
na mikwaju 82 na Lina Nkya handicap 15 alishika nafasi ya pili baada ya kurejea
na mikwaju 88.
Kwa
upande wa kundi la wanawake Tayana William handicap 24 aliibuka mshindi kwa
kupiga mikwaju 72, akifuatiwa na Vailet Peter handicap 13 akiwa na mikwaju 74
na Vicky Elias handicap 13 alishika nafasi ya tatu baada ya kurejea na mikwaju
76.
Mbali
na wachezaji wa ridhaa mashindano hayo pia yalihusisha kundi la wachezaji wa
kulipwa ambapo Geofrey Leverian alirejea na mikwaju 75 gross na kuibuka mshindi
wa kundi hilo lililohusisha wachezaji 18. Nafasi ya pili na tatu ilikwenda kwa
mchezaji mkongwe Mbwana Juma na Nuru Mollel waliopiga mikwaju 76 na 77.
Kwa
upande wake muasisi wa michuano hiyo Mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George
Waitara aliwashukuru washiriki wote kwa kuonyesha ni jinsi gani wameendelea kuthamini
michuano hiyo na kuwataka kuendelea na moyo huo.
Waitara
pia alitumia nafasi hiyo kuishukuru Kampuni ya bia ya Serengeti na kumpongeza
Mkurugenzi Mkuu (mstaafu) wa Kampuni hiyo Bw. Steve Ganon ambaye mara zote
hakusita kudhamini michuano hiyo na kuomba wadau wengine kuiga mfano huo.
Naye
Mgeni rasmi wa michauano hiyo Jaji (Mstaafu) Mark Bomani alitoa changamoto ya wadau
wa mchezo huo kushiriki katika kuongeza viwanja vingi zaidi vya mchezo huo huku
akianisha maeneo kama Dodoma, Mwanza na Mbeya ambapo wadau hao wanaweza
kuendeleza mchezo huo.
Mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi
mstaafu Jenerali George Waitara huandaliwa na kufanyika kila mwaka kwa
madhumuni ya kuenzi mchango wake wa kimichezo nchini kwa kuasisi uwanja wa gofu
wa Lugalo golf club. Uwanja huo ulianzishwa mwaka 2006 kwa mchango mkubwa
uliotolewa na Jenerali mstaafu George Waitara kipindi alichokuwapo madarakani,
pia kuendelezwa na Mkuu wa Majeshi aliyefuata na aliyeko madarakani kwa sasa Jenerali
Davis Mwamunyange
No comments:
Post a Comment