18 October 2015

DIAMOND KUSHINDANA NA MREMBO KUTOKA INDIA PRIYANKA CHOPRA KWENYE MTV EMA 2015



Nyota ya Diamond Platnumz inazidi kung’aa na kumulika hadi nje ya bara la Afrika ambako pia imeanza kukubalika.
 
Siku chache baada ya kushinda tuzo za AFRIMMA, 2015 na Best African Act (MTV 2015), msanii huyo mzawa wa Tandale, Dar es Salaam sasa atashindana na magwiji wa burudani wanaowakilisha kanda mbalimbali duniani akiwemo mrembo wa dunia wa mwaka 2000, kutoka India, Pyanka Chopra akiwa mshindi wa tuzo ya Best Indian Act.

Diamond na Pryanka Chopra watashindania kipengele cha Worldwide Act EMA katika tuzo hizo zinazoandaliwa na MTV!
 
Muigizaji wa filamu, muimbaji na aliyekuwa Mrembo wa Dunia (Miss World 2000), Priyanka Chopra.
Priyanka Chopra ni mwanamuziki mrembo mwenye umaarufu mkubwa duniani ambaye tangu ashike taji la mrembo wa dunia aliacha alama ambazo hazifutiki kwenye historia ya mashindano hayo.
 
Pia, amefanikiwa kuzing’arisha filamu nyingi na kubwa za kihindi na hivi sasa anashiriki katika tamthilia maarufu ya Marekani ya Quantico inayooneshwa na kituo cha ABC.
 
Diamond na Priyanka watashindana na washiriki wengine kutoka Australia, New Zealand, Ulaya, Latin America na Marekani Kusini.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname