11 September 2015

Ulishawahi kujiuliza kwanini Jay Z hayupo kwenye mitandao ya kijamii? Hili ndio jibu


Rapper na mmiliki wa label ya “Roc Nation” Jay Z si mpenzi wa mitandao ya kijamii, Siku chache zilizopita alijiunga na mtandao wa Instagram lakini aliifuta baada ya masaa 24, Pia yupo kwenye mtandao wa Twitter lakini ametweet mara 236 na mara ya mwisho ilikua November 2008.
Rappa MeekMill amefunguka vitu alivyowahi kuambiwa na Jay Z kuhusu mitandao ya kijamii na ndio inaweza ikawa sababu kubwa ya rappa huyo kutoitumia.                                               Jay Z na Meekmill
“Jay Z aliwahi kuniambia kuwa mitandao ya kijamii imewekwa kwa sababu ya wale watu ambao hata ukikutana nao hawawezi kuongea kitu, watu ambao wanaogopa  kuongea moja kwa moja na wanawake au wanaume (kutongoza) na huwezi kuongea ukweli sababu mitandao ni dunia ya watu fake na watakuchukia ukisema ukweli, Watu hawana maisha tena sababu wana dunia ya kuigiza kuwa wana maisha bora” Meekmill alisema.
Kwa maneno hayo ni sababu za wazi kwanini Jay Z si mpenzi wa mitandao ya kijam

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname