![]() |
| JULIUS MTATIRO |
thechoice ilishuhudia Makada hao wa CHadema Bi Annatropia THEONEST na Mwenyekiti wa Jimbo hilo Gado Kidera wakigongana kwa Mkurugenzi wakirejesha fomu za kugombea jambo lililosabbisha wapambe wa Makada hao washikane mashati huku kila mmoja akidai mtu wake ndiye anayestahili kurejesha Fomu.
Katika uchaguzi wa kura za maoni ndani ya chama hicho Bi Theonest aliibuka kidedea wakati huo Bwana Kidera alishika nafasi ya 6.
wapambe wa Theonest wameeleza kuwa Chadema Makao Makuu walitoa barua kwake ya kumteua kuwa Mgombea wa Jimbo hilo lakini wanashangaa kujitokeza Kidera ambaye alishindwa vibaya kwenye kura za maoni.
Hata hivyo wapambe hao wa Theonest wameulaumu uongozi wa chama hicho Makao Makuu kwa kuchelewa kumpa barua ya utambulisho kwani barua hiyo iliandikwa tarehe 17 Julai lakini ameipata terehe 20 Agost tena kwa kuifuatilia mwenyewe.
Mgombea wa Chama hicho Jimbo la Ukonga Mwita Mwikabe Waitara ameshutumiwa na wanachama wenzake kwa kukihujumu chama kwa kumshawishi Kidera kujaza fomu na kuzirudisha mapema kwa Mkurugenzi huku akijua hana baraka za chama Jimboni na MAKAO makuu.
Wanachama hao wameonekana wakimburuza Waitara kama mwizi kwenye viwanja vya Manispaa ya Ilala Anaultoglo wakidai kumuona akiambatana na Kidera na kumwelekeza taratibu zote za kurejesha fomu
wakati huohuo, Bwana Julius Mtatiro wa CUF naye amerudisha fomu kwa ajili ya kugombea Jimbo hilo kwa kile kinachodaiwa ni makubaliana ya UKAWA ya kuachiana Majimbo na kwamba Jimbo hilo liliangukia kwa CUF katika mgawanyo huo.
Hadi mtandao huu unaondoka eneo la tukio majira ya Saa 9:30 alhasiri muafaka ulikuwa haujafikiwa wa fomu za nani zichukuliwe kati ya Anna (mwenye Barua ya utambulisho) na Kidera ambaye alikuwa ameishaondoka baada ya fomu zake kukubaliwa. Mkurugenzi alikuwa anasubiri maelekezo ya Makao Makuu ya CDM kuhusu uhalali wa wawili hao kabla ya muda wa kurejesha fomu hizo kuisha ambao ulikuwa ni saa 10 kamili jioni.

No comments:
Post a Comment