Waziri Mkuu Mstaafu Frederick Sumaye mchana huu anatarajiwa kujiunga na Chama Cha NCCR-Mageuzi katika kile kinachoitwa "Mpango Mbadala" kutokana imani ya viongozi wa UKAWA kwamba lolote litatokea kwa Mgombea wa UKAWA kutokana na hali yake ya afya kuendelea kutetereka kwa kasi.
Mazungumzo kati ya UKAWA na Bwana Sumaye yamechukua uharaka mpya hivi karibuni kutokana na ukweli kwamba katika kipindi hiki kifupi ambacho viongozi wa UKAWA wamekuwa karibu na Bwana Lowassa ndipo wameshuhudia ukubwa wa tatizo lake la afya na katika vikao ambavyo havikumhusisha Lowassa wamejiridhisha kwamba hataweza kufanya kampeni nchi nzima kwa ufanisi na kwamba, hata kama wakishinda uchaguzi, Bwana Lowassa hatakuwa na uwezo wa kuendesha Serikali.
No comments:
Post a Comment