Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete, Mama Salma Kikwete (Picha na Mtandao).
Ilikuwaje? Taarifa ikufikie kuwa, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth
Michael `Lulu’ aliibua minong’ono kwenye msiba wa mwanamuziki Ramadhan
Masanja `Banza Stone’ baada ya kutaka kumsalimia kwa kumshika mkono mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete,
Mama Salma.
Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael `Lulu’.
Chanzo chetu kilichoshuhudia tukio hilo lililojiri hivi karibuni
kilisema kuwa Lulu aliingia nyumbani kwa wazazi wa Banza, Sinza-Lion,
Dar ili kuwasalimu wafiwa lakini baada ya kumuona Mama Salma Kikwete
alijisogeza jirani kwa lengo la kutaka kumsabahi lakini walinzi wake
walimzuia kwa kuwa ni kinyume na utaratibu.
Baada ya kubwagiwa ‘ubuyu’ huo, Ijumaa Wikienda lilimvutia waya Lulu
ambapo awali alidai hakumuona msibani hapo, lakini baadaye alikiri
kumuona ila hakupata fursa ya kumsalimia naye.
No comments:
Post a Comment