26 July 2015

LEMA AFUNGUKA LIVE: TUTAMPOKEA KIGOGO WA CCM,TETESI ZA KIGOGO HUYO ZIKO HAPA


Mbunge wa Arusha Mjini,Godblees Lema, amesema watapokea "kigogo mkubwa" kutoka CCM pamoja na wenyeviti wa mikoa na wilaya katika mkutano utakaofanyika Dar-es-salaam.
Mkutano huo utafanyika wiki ijayo kwa mujibu wa taarifa hiyo.Shinikizo dhidi ya Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, la kumtaka akihame Chama Cha Mapinduzi (CCM) linazidi kuongezeka na katika timu yake ya ndani ni watu wawili tu wanaonekana kumtaka abakie ndani ya chama hicho. Habari za ndani ya vikao vya kujadili hatua za kuchukuliwa na Lowassa baada ya jina lake kukatwa kwenye mchakato wa kugombea urais kupitia CCM, zinasema kuwa wandani wake wanaamini kuwa hana atakachopata kama ataendelea kubaki kwenye chama hicho tawala. 



No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname