Mtangazaji mwenye sauti nzito Bongo kupitia Clouds FM, Millard Ayo,
Jumatatu iliyopita alibanwa azungumzie uhusiano wake na warembo wenye
majina makubwa nchini, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Jacqueline Wolper na
Elizabeth Michael ‘Lulu’ ambapo alimfungukia mmojammoja.
Katika mahojiano maalum na Kipindi cha Sporah Show, mtangazaji alimbana
Millard akimtaka aseme ukweli kuhusu warembo hao ambapo alianza kwa
kumzungumzia Lulu kuwa hajawahi kuwa mpenzi wake zaidi ya kumfahamu
katika sanaa.
“Kuhusu Lulu! Hapana sijawahi kabisa kuwa na uhusiano naye. Yaani hata
kuwaza sijawahi. Namfahamu kuwa ni mwigizaji na ni mtu ambaye nimekuwa
nikimfuatilia kupitia kazi zangu za utangazaji,” alisema mtangazaji huyo
staa.
Millard aliendelea kupangua, ikafika zamu ya Wolper. Alikana vikali kuwa naye hata kujuana kwao si kwa ukaribu. Alisema:
“Haa! Wolper ndiyo kabisa, nimekuwa nikimuona na kumsikia tu, wala
sikuwahi kumuwazia kwa lolote lile isipokuwa ninamjua kama msanii wa
Bongo Muvi na huwa nakutana naye kama ninavyoweza kukutana na mtu
mwingine yeyote ambaye hatujuani.”
Kwa upande wa Jokate, hapo alipiga kituo kidogo na kuanza kumzungumzia
kwamba, amemfahamu miaka mingi na alikuwa akimpenda kama ‘girl friend’
wake kwani wakati anasoma alishawahi kupanda naye daladala na wakapiga
stori.
“Nampenda Jokate kwa sababu mpole, anatoka katika familia ya
wachakarikaji, hivyo nimekuwa nikimshirikisha katika mambo yangu.
Nampenda kwa sababu hiyo ila huwezi kuamini, nilipotezana naye na
baadaye tumekuja kukutana tayari yeye ni maarufu na sikuwahi kumwambia
chochote juu ya kumpenda kwangu kwa kuwa tayari ana ‘boy friend’ wake.
“Jokate naye anamjua mchumba wangu ingawa hajawahi kumuona. Kwa sasa
namchukulia kama dada yangu tu kwa kuwa hakuna popote ambapo nimewahi
kutoka naye kimapenzi hata kwa dakika moja zaidi ya kuwasiliana naye
kikazi. Mara kadhaa nimekuwa nikimtafuta hata kama ni usiku wa manane
nikiwa na jambo na huwa sisiti kumshirikisha,” alisema Millard.
Kwa upande wa Jokate baada ya kufikishiwa taarifa ya maneno ya Millard
alishangaa, akasema yeye hajui chochote. Kwanza aliwekewa mtego kama
angeuingia kwa kuambiwa Millard amemtaja yeye kuwa ni mchumba wake,
akashtuka na kusema:
“Huh! Kasema hivyo lini? Maana mimi sijasikia lolote na siyo kweli kama
ni mpenzi wangu na sijui kwa nini kaongea hivyo. Kwa kweli sijasikia
wala kuongea naye.”
Wolper yeye alipoulizwa juu ya maneno ya Millard kwamba hawajahi kuwa
karibu kwa jambo lolote zaidi ya kuonana barabarani alishtuka:
“He! Ni kweli lakini. Hata mimi namwonaga tu. Hivi yupo kwani hapa Bongo? Sina koneksheni ya kitu chochote na yeye.”
Lulu alipotafutwa juzi, simu yake iliita kwa muda mrefu lakini hakupokea.
Kuhusu Millard na Jokate, baadhi ya vyombo vya habari vimewahi kuripoti
kuwa wako karibu kiasi kwamba, maswali ni mengi kuliko majibu.
Kwenye ‘bethidei’ ya Millard iliyofanyika Januari 26, mwaka huu nyumbani
kwake, Ubungo Msewe jijini Dar, Jokate alishiriki kwa kumpelekea keki
ya ‘kumuwishi’ ambayo ilizua utata
No comments:
Post a Comment