JACQUELINE WOLPER: MIMI NI FREEMASON KWA MUDA MREFU SASA
Staa
wa bongo movie Jacqueline Wolper Massawe ‘Twiga wa Jangwani’. UPO?
Mtoto mzuri katika tasnia ya uigizaji Bongo, Jacqueline Wolper Massawe
‘Twiga wa Jangwani’ amesema haoni sababu ya kuukana uanachama wa taasisi
ya Wajenzi Huru (Freemason) kwani ni dini kama zilivyo zingine na kama
katiba inavyoelekeza, kila mtu anayo haki ya kujiunga na dini au taasisi
yoyote ya kuabudu kulingana na matakwa ya imani yake.
Jacqueline
Wolper Massawe akiwa katika pozi. Akichezesha taya na Amani, Wolper
alisema ni kweli yuko katika kundi hilo huku akishangaa watu kustaajabu
kuona mtu yuko Freemason wakati walioanzisha dini hiyo ni binadamu kama
wengine.
“Freemason si ni taasisi au
dini kama zingine? Kuna ajabu gani mimi kuwa mwanachama? Tena nataka
nikuhahakikishie kuwa, nimekuwa muumini halisi wa Freemason kwa muda
mrefu sasa,” alisema Wolper
No comments:
Post a Comment