25 June 2015

Faiza Akata Rufaa Dhidi ya Ushindi wa Sugu, Asema Atamlea Mtoto Wake na Kuvaa Mavazi Yake!

http://www.bongomovies.com/public/uploads/faiza22.JPG

Staa wa Bongo Movies, Faiza Ally aliyekuwa mchumba wa mbunge wa Mbeya Mjini, Mh Joseph Mbilinyi ‘Sugu’  amekata rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa hivi juzi ambayo ilimpa ushindi Sugu na hivyo kumchukua mtoto (Sasha) baada ya Faiza kuonekana kuwa ana muharibu mtoto kutokana na tabia zake ususani mavazi.
Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa instagram, Faiza mbali na kuelezea rufaa yake ameeleze pia masikitiko yake kutokana na baadhi ya watu kumshabulia kwa maneno makali  juu ya mavazi yake bila ya kujua kuwa yeye ni mama bora.
“Nasitikishwa sana na maneno yenu makali hasa nyinyi mnao sambaza kashfa juu yangu kuhusu mavazi yangu” Akaendelea
“Hakuna hiyo sheria Tanzania inayosema nipokonywe mtoto kuhusu mavazi yangu. Nimekata rufaa na nawahakikishia nitashinda kesi na nitamlea mwanangu na nitavaa mavazi yangu na nita enjoy maisha yangu/ nina mwanasheria makini aliesomea sheria na sisi nyinyi mnao nipa hukumu humu ndani na kwingine! “
Akasisitiza,
“Pamoja na mavazi yangu mimi ni mama bora! mnajua upande wangu lakini hamjui upande wa Sugu na hakika mengi mtayajua kupitia kesi hii/ mavazi yangu nayapenda na kwa mujibu wa sheria si kitu kinacho nifanye ni pokonywe mtoto wangu”
Akili kuumizwa na maneno lakini hayatamrudisha nyuma
“Maneno yenu machafu dhidi yangu yananiuma sana lakini kamwe hayata nirudisha nyuma katika kutetea haki yangu! namjua Sugu na na ninajiua mimi katika ubora wangu katika malezi ya mwanangu/ mimi ni mama na si mama tu ni mama bora kwa Sasha na ananihitaji na sitamuacha na nyinyi wajinga wachache endeleeni kuniponda na kuona na stahili kupata pigo hili na si wote”
Akamalizia na kushukuru wanaompa moyo na kumuunga mkono
“Kuna wengine wema kwa upande wangu na washukuru na nina waahidi sitawarudisha nyuma nitasimama mpaka kieleweke- sasa hivi ni jasiri kupita maelezo ....in god we trust inshaallah

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname