22 May 2015

SHOPPING YA MTOTO WA DIAMOND KUFURU TUPU!!,SHUHUDIA HAPA


Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akifanya shopping ya mtoto wake anayetarajiwa kuzaliwa.
KITU CHA DUBAI NA LONDONKAMA ulishawahi kusikia neno kufuru na ukajua maana yake, basi ndiyo imefanywa na Mwanamuziki Bora wa Afrika Mashariki na Kati, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, baada ya kuteketeza mamilioni ya fedha kwa ajili ya kufanya ‘shopping’ ya nguo na vifaa mbalimbali vitakavyotumiwa na mwanaye ikiwa ni siku chache kabla mpenzi wake, Zarinah Hassani ‘Zari The Boss Lady’ kujifungua.
Akizungumza na Ijumaa mapema wiki hii, mtu wa karibu wa Diamond anayekuwa naye popote anapokwenda alisema kuwa shopping hiyo aliifanya juzikati huko Dubai na jijini London, Uingereza ambako alikwenda kufanya shoo yake ya Diamonds Are Forever.
Alisema kuwa, akiwa London baada ya shoo, Diamond aliona ni vema akafanya manunuzi hayo kwani hivi karibuni atapata mgeni (malaika) kwenye familia yake.
KUMBE ALIANZA KITAMBO
Mtu huyo aliendelea kunyetisha kwamba, Diamond alinunua vitu vingi zaidi ya hivyo ambavyo alivipiga picha kwani hata kabla ya kununua huko London tayari kuna baadhi alinunua njiani na kuna siku alinunua vingine jijini Dar.
Alisema kuwa kwa harakaharaka hadi sasa vitu ambavyo Diamond ameshanunua ukivipigia gharama ni zaidi ya Sh. milioni 10 za Kitanzania.‘Diamond Platnumz’ akishika tumbo la Zari.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname