
Kwa mujibu
wa chanzo makini, Wema amekuwa akitumia kilevi hicho kwa muda mrefu huku
akifanya jambo hilo kwa siri kubwa.“Hivi hamna habari ya Wema kubwia
unga? Mbona kila mtu anajua, watu wengi tu wanafahamu lakini wanashindwa
namna tu ya kumueleza mwenyewe ili aache maana kila mtu anamhofia si
unamjua naye Madam mtu wa kumaindimaindi,” kilisema chanzo hicho.
Kama
hiyo haitoshi, kwa nyakati tofauti, watumiaji mbalimbali wa mitandao ya
kijamii wamekuwa wakidai kuwa staa huyo anabwia unga licha ya kuwa
hawana ushahidi wa moja kwa moja.“Mimi sijawahi kumuona lakini kuna watu
wake wa karibu tu wananihakikishia kwamba Wema anatumia madawa ya
kulevya, ila naamini mwenyewe anaujua ukweli wote wa haya yanayosemwa,”
ilisomeka sehemu ya maoni mtandaoni.
Baada ya kupata madai hayo, Risasi Jumamosi lilimfungia kazi Madam ili kuweza kumsikia anazungumziaje tuhuma hizo nzito.
No comments:
Post a Comment