- Ameweza kujijengea himaya ndani ya kanisa lake kwa kutumia udhaifu wa baadhi ya waumini aidha kwa kuwa na uelewa mdogo wa imani ama kutokana na kupigwa kimaisha. Wengi wao amewawezesha kimaisha na akaweza kujiaminisha kwao kuwa yeye ndo tegemeo la maisha yao na bila yeye imani yao kwa Yesu Kristo ni bure. Na hawa ndo waliomzunguka na pengine kujifanya washauri na jeshi lake.
- Kutokana na matatizo yaliyoko kwenye familia nyingi na udhaifu wa wake ama dada zetu ambao wamekuwa wepesi kuweka mambo yao wazi kwa huyu Gwajima bila kujua yu “opportunist” wakitegemea msaada wa kichungaji kuondokana na matatizo waliyo nayo. Hali imekuwa ni tofauti na matarajio yao kwani Gwajima na baadhi ya washauri wake wa karibu wamekuwa wakitumia mwanya huo kujipenyeza kwende maisha yao kwa kuanzisha nao mahusiano ya mapenzi kwa namna ambavyo huwezi kugundua kwani muda mwingi amekuwa akijinasibu kwao kama “Baba wa Kiroho”.
- Ikitokea una mke ama mchumba akikutana na Gwajima ujue hiyo ndoa ama uchumba lazima uvunjike. Kuna mifano mingi ya tangu mwaka 2010 kwa ndoa na uchumba uliovunjwa na Gwajima kwa maslahi ya kanisa ama kwa maslahi yake binafsi. Kuna hata ndoa ya mheshimiwa mmoja na mwimbaji ambayo ilikuwa ifanyike kama mwaka mmoja uliopita ikashindikana. Kama mtakumbuka mheshimiwa huyo alisema kulikuwa na kikundi cha maombi kuombea ndoa ifungwe ama isifungwe na inasemekana wana maombi walikuwa waumini wa Gwajima kwani Mh huyo ni muumini ama aliwahi kuwa muumini wake na aliwahi kuimba wimbo mmoja mzuri sana. Hivyo ndo mwelewe Gwajima akimnasa mke ama mchumba wako huna lako. Yasemekana Mh huyo naye aliwahi kunasa kwenye anga za Gwajima ingawa mahusiano yao hayakuwa wazi.
- Wengi ya waumini wake wako pale kutokana na hofu kwani mafundisho yake mengi ni kuwajengea watu hofu na wengi huamini bila Gwajima hakuna namna ya kukua katika imani ya Kikristo pasipo kung’amua kuwa huyu jamaa ni “opportumist”.
- Amekuwa na utaratibu wa kuandaa mikutano mikoani kama alivyowahi kufanya Morogoro, Moshi, Arusha, Iringa, Mtwara na Tanga. Akiwa huko mikoani amekuwa na utaratibu wa kukutana na waumini wake muda wa usiku baada ya shughuli za mikutano hiyo na wengi wao ni wale anaosafiri nao toka huku Dar. La kusikitisha akiwa huku Dar kuonana naye imekuwa si rahisi labda itokee kuwasiliana kwa simu kutokana na ukiritimba wa washauri/ walinzi wake. Hivyo kuweza kuwanasa ama kutekeleza mipango yake na wake za watu ama dada zetu basi hufanya jitihada za kusafiri nao.
- Kinachosikitisha ni kuwa inaonekana amewapumbaza kabisa waume/wake/dada zetu kwani wakiisha kuingia kwenye mikono ya Gwajima basi ujue si ndoa wala uchumba tena. Kila kitu ni Gwajima - sijui huwa anawawekea nini hawa waumini wake. Moja ya mafundisho yake ni kuwa “kiongozi wako wa kiroho” akikosea hutakiwi kumuuliza ama kumkemea zaidi sana amewataka wawe wanamwachia Mungu adeal nao kwani ndo aliyempatia huo “Umasihi”. Tujiulize mbona yeye Gwajima hakumwachia Mungu adeal na Askofu Pengo akaishia kumtolea lugha za kuudhi?
- Ikitokea ukikwaruzana na mwenzi wako kwa ajili ya yeye kuingilia mahusiano yenu ya ndoa/ uchumba huwa anahakikisha kwa gharama yoyote anawavuruga na mara nyingi amekuwa akiwashawishi kwa misaada ya kifedha, magari, nyumba ama viwanja.
- Kikundi chake cha propaganda ni hatari kwani wakiisha kumpata mwenza wako humganda kiasi asiweze kufikiri nje ya wanachokitaka. Hatari ni kuwa hawa jamaa wanauwezo wa kukufanya lolote kwani huamini kwa kufanya hivyo wanamtumikia vyema “Masihi wao Gwajima”.
Ombi na ushauri kwa jamii:-
- Tunaomba maaskofu na wachungaji mfunge kwa sala kuombea hili janga la mwenzenu anavyoingilia mahusiano (ndoa/ uchumba) katika jamii. Huu si ukristo mnaoutangaza!
- Imekuwa tabia ya Gwajima kutoka na wake za watu kwenda mbali ya nyumbani akifikiri watakachofanya itakuwa siri lakini ajue yote yako wazi. Wahusika wengi yawezekana wameamua kutoyaweka wazi kwa jamii na kufanya siri kwa kulinda haiba zao
- Wanaopenda kusafiri na Gwajima kwenye huduma zake za ndani na nje ya nchi basi jihadharini. Si kila utakachoambiwa na Gwajima ni sawa mbele za Mungu. Simamieni imani zenu – kumbukeni kuwa hamumtumikii Gwajima bali mnapaswa kumtumikia Mungu wa Israel maana inawezekana mwenzetu anaye Mungu wake ambaye njia ya kumfikia ni kupitia yeye Gwajima. Mungu wa Israeli kumfikia ni kupitia Yesu Kristo tu.
- Wale wanaomzunguka Gwajima ambao kwa namna moja ama nyingine amewanunulia magari ama kuwapangishia nyumba (kuwawezesha kiuchumi) na pengine mmeahidiwa kupewa nyumba ama viwanja bado mnayo nafasi ya kusimamia imani yenu katika Ukristo. Mwombeni roho awaongoze msidanyanyike na mali kwani zote mtaziacha hapa hapa duniani.
- Wale ambao kwa namna moja ama nyingine ndoa zenu zimeathiriwa ama kuingiliwa na Gwajima yawapasa mumlilie Mungu na mtubu kwa kumruhusu shetani maishani mwenu. Kumbukeni mlikotoka na mnako kwenda na wajibu wenu kwa familia zenu mbele za Mungu uko pale pale. Msijishike na Gwajima kama nguzo ama hirizi wakati wa dhoruba kwani naye atajibu yote mbele za Mungu.
- Mwombeni Roho wa Mungu awafunulie maandiko na tafsiri sahihi toka kwake na msitegemee tafsiri potofu zinazotolewa na Gwajima kwa lengio la kucover mambo yake.
- Zaidi sana tufunge na kumwomba Mungu azidi kubariki familia zetu na kutuwezesha kukua kiroho.
- Muwekeni Mungu wa Israeli kuwa tegemeo lenu – msimtumie Gwajima kama msoma ramli ama mafundisho yake kuhusu maisha yenu zaidi jishikeni na Yesu Kristo nanyi mtapata uponyaji.
- Kama Wakristo ni wajibu wetu kutambua kuwa ni zaidi ya miaka elfu mbili baada ya Yesu Kristo sasa walikuwepo/ wapo/ watakuwepo “Masihi” wengi na kutafsiri Biblia takatifu kwa namna walivyoongozwa na Mungu ama Miungu yao kwa maslahi mapana ya kilichowasukuma na bado “NENO LA MUNGU” li hai hata sasa “UNEDITABLE”.
HUYU NDIYE GWAJIMA ANAYEJINASIBU KUIENDELEZA NA KUIHUBIRI INJILI YA YESU KRISTO PASIPOKUJALI WAJIBU WAKE WA HUDUMA YA KIROHO KWA WANAOKUJA KWAKE KWA MSAADA WA KIROHO BADALA YAKE AMETEKWA NA TAMAA ZA KIMWILI.
TAMBUENI KUWA NA KARAMA YA UPONYAJI HAINA MAANA YU MTAKATIFU KAMA WENGI MNAVYOFIKIRI NA HIYO NI KUTOKANA NA UVIVU WA KUSOMA NENO LA MUNGU - BIBLIA NA KULIELLEWA KITU AMBACHO NI UGONJWA WA WAKRISTO WA LEO TUNAOTAKA KUSIKIA MAONO YA MAISHA YETU KUPITIA KWA MTUMISHI YULE BADALA YA ROHO WA MUNGU.
Mathayo 28:18 - 20
No comments:
Post a Comment