Baada ya mkuu wa jeshi la
polisi nchini kuvipiga marufuku vyama vyote vya siasa kuwa na makundi
ya kujihami katika vyama hivyo, CHADEMA wamekaidi agizo hilo halali la
polisi na wameendelea kuwatumia Red Brigedi katika chama chao.
Zifuatazo ni picha za vifaa vya kijambazi vilivyonaswa na jeshi la polisi.
Mnamo tarehe 24/4/2015 huko
maeneo ya Sogea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, METHEUS ANGANILE
MWAFONGO, Mndali, 37yrs, Mkuu wa Ulinzi CDM Wilaya Momba, pamoja SALEHE
TABLEI@SICHALWE, 22yrs, mkazi wa Majengo Tunduma walikamatwa kutokana
na taarifa za kiintelijensia.
Watu hawa walikamatwa
wakiwa na buti pair 2 za kijeshi, kofia pair 2 za kijeshi, kamba kurukia
ya mazoezi, vyuma kwa ajili ya mazoezi ya pushup, visu pair 2 kimoja
spring knife na kingine kisu kikubwa, miwani ya FFU(ya kwenye misafara),
manati pair 2 na mawe yake 40 pamoja na nati 4 zilizotarajiwa kutumiwa
kama mawe, shenguard kwa ajili ya mikono na miguu pair 4, Bendera 2 za
CDM, Tshirt 1 ya CDM, Kilemba 1, koti 1, Pamoja na barua 3 za CDM za
kata ya MSANGANO, SHITETE, na KAMSAMBA (W) MOMBA zenye kichwa cha habari
"UTOAJI WA VIONGOZI WA RED BRIGED KATIKA KATA YENU KWA MAFUNZO YA RED
BRIGED".

Barua inasomeka hivi
Husika na kichwacha barua hapo juu chajifafanua vema.
Napenda kukujulisha kuwa
kutakuwa na ziara ya kimafunzo ya RB (Red Briged) katika kata yenu kwa
ajili ya maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Na kwa barua hii naomba uwapokee na uwape ushilikiano wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya chama chetu.
Ni matumaini yangu kuwa utawapokea na kuwatunza pamoja na usalama wao.
Wako katibu wa chama Wilaya.
No comments:
Post a Comment