Mshindi wa mwisho wa shindano la “Tutoke na Serengeti” Bw.Gabriel Robert Moriale (Kulia) akiwa na kaka yake Bw.Joshua Robert Moriale (Kushoto) walipowasili mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro jijini Arusha tayari kwa kuanza safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kukamilisha mtoko wao wa siku tatu ndani ya hifadhi hiyo. Robert aliibuka mshindi wa mwisho wa “Mtoko wa mbugani” baada ya kushiriki kwenye kampeni ya “Tutoke na Serengeti” iliyoendeshwa na kampuni ya bia ya Serengeti kwa ushirikiano na BPESA kwa takriban miezi(4) ambapo washindi walijinyakulia zawadi nyingine kama Limo Bajaj, fedha taslim, Bia za bure sambamba na punguzo la Tsh.300 kwenye bia ya Serengeti Premium. |
No comments:
Post a Comment