21 April 2015

MASHABIKI WAMUOMBA KADINDA ASAIDIE KUWASULUHISHA WEMA NA KAJALA

 
Mashabiki na wadau mabalimbali wamemuomba Martin Kadinda amabe ni meneja wa Staa Wema Sepetu, asaidie kuwapatatisha wema na Kajala ili warudi kuwa karibu kama zamani.
Mashabiki na wadau hao walimwaga komenti za ombi hilo kwenye ukurasa wa Kajala mtandaoni mara baada ya kajala kubandika picha akiwa na Kadinda na kuonekana wanafuraha.
“ Kweli martin jaribu kuwaweka sawa i know wema ni mtu mwenye moyo wa huruma sana atamsamehe tu mshawishi” mmoja alikomenti akimsisitiza Kadinda.
Mbali na kuwa Wema na Kajala wapo kwenye mtafaruku, lakini Kadinda amekuwa akionekana kutoingilia ugomvi wao na kuendelea kuwa na urafiki na Kajala japo kuwa yeye ni meneja wa Wema Sepetu.
Bila shaka maombi hayo ameyapata.
Mzee wa Ubuyu

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname