Stori: Mwandishi Wetu na Mitandao
WAKATI binadamu wakiendelea na mipango yao ya kuifanya dunia kuwa
sehemu salama ya kuishi kimazingira, kiulinzi na usalama, utabiri mpya
wa kutisha unaonesha kuwa mwaka 2032 ndiyo mwisho wa sayari hii ya tatu
katika mfumo wa jua.
Kwa
mujibu wa vyanzo mbalimbali katika mitandao ya internet, sayari iitwayo
Nibiru, ambayo kisayansi inafahamika kama Planet X ipo njiani kuigonga
dunia na hivyo kusababisha majanga mbalimbali kutokea.
ITAONEKANA ANGANI KAMA MWEZI
Kwa mujibu wa
mitandao hiyo ya kisayansi, sayari hiyo ambayo inaisogelea dunia kwa
kasi kubwa, itaonekana kubwa na angavu wakati wa usiku angani na kuwa
katika umbo la mwezi na hivyo kufanya miezi ionekane miwili.
DALILI KWAMBA IPO JIRANI
Taarifa zaidi za
kisayansi zinasema kuwa, kadiri sayari hiyo inavyozidi kusogea, dunia
itaanza kutikisika na kusababisha matetemeko ya ardhi kuongezeka sehemu
mbalimbali.
Mbali na dunia kutikisika na matetemeko, milipuko ya volcano nayo
itatokea huku idadi kubwa ya milipuko hiyo mipya ikiongezeka, vimbunga
vikubwa kama Tsunami vitaibuka na mwishowe dunia itapigwa na bomu la
miamba midogo na vimondo kutokea angani.
DUNIA ITAKUMBWA NA GIZA NENE
Wakati volcano zote
duniani zitakapoanza kulipuka na zingine mpya kujitokeza, dunia
itafunikwa na giza nene na matope kwa wakati wote wa usiku na mchana
huku watu wakitakiwa kusoma katika Biblia Joel 2: 1-2 na Zephaniah
1:14-17.
NI TUKIO LA AINA YAKE KARNE YA 21
Nibiru
inatajwa kama kitu kinachoisogelea dunia kinachoaminiwa kusababisha
madhara makubwa ambapo kama hakitaigonga dunia, kitasababisha mtikisiko
usio wa kawaida kitakapopishana nayo. Baadhi ya wanasayansi wanaamini
kuwa kitendo hicho kitatokea mapema katika karne ya 21 (tuliyonayo
sasa).
WANASAYANSI WAPINGANA
Baadhi ya wanasayansi
wanapinga kwa maelezo kwamba hakuna ushahidi wowote wa kitafiti
unaoonesha wazi kwa mabingwa wa anga za juu waliobobea wa masuala ya
nyota.
MWANAMKE ALIWAHI KUOTA NDOTO
Kwa mara ya kwanza
jambo hilo lilitokea mwaka 1995, wakati mwanamama Nancy Lieder muasisi
wa mtandao wa ZetaTalk, aliwahi kudai kuoteshwa ndoto kwamba, Mei 2003
kuna kitu kitaingilia mfumo wa jua (solar system) na kusababisha dunia
kutoboka tundu litakalosambaratisha sehemu kubwa ya kizazi cha binadamu.
Lieder aliifafanua kuwa, kitu hicho kitakuwa na ukubwa wa mara nne ya dunia.
BAADA YA NDOTO
Baada ya mwanamama Lieder, mtu wa
kwanza kuizungumzia Nibiru alikuwa Mark Hazlewood, mwanachama wa zamani
wa mtandao wa ZetaTalk ambaye mwaka 2001 alichapisha kitabu kilichoitwa
Blindsided na kusema kuwa mwisho wa dunia ungekuwa mwaka 2003 baada ya
kuwasili kwa sayari ya kumi (Nibiru).
Katika mfumo wa sasa, baadhi ya wanasayansi wanasema sayari ziko 12,
wakizitaja kwa namba 1. Jua 2. Mercury 3. Venus 4. Dunia 5. Luna (mwezi)
6. Mars 7. Jupiter 8. Saturn 9. Uranus 10. Neptune 11. Pluto 12.
Nibiru.
IMANI NYINGINE YASEMA MWISHO WA DUNIA NI FEBRUARI 22, 2014
Hata hivyo, utabiri mpya uliotolewa na watu wa jamii ya Vikings jijini
New York, Marekani umesema mwisho wa dunia ni Februari 22, mwaka huu.
Mitandao mbalimbali pamoja na gazeti maarufu la Daily Mail la
Uingereza lilielezea utabiri huo uliofanywa na jamii hiyo ukidai kuwa
mwisho wa dunia utatokana na Mungu Odin kupigana na kuuawa na shetani
Wolf Fenrir, hivyo kuiachia dunia anayoishikilia.
Wamesema baada ya kuiachia dunia itafurika maji ambayo yatakuwa na sumu, hivyo viumbe wote watateketea.
WATUMISHI WA MUNGU TANZANIA
Baadhi ya watumishi
wa Mungu nchini wamekuwa wakisimamia andiko la kwenye Biblia linalosema
kuwa, hakuna mwanadamu anayeijua siku wala tarehe ya mwisho wa dunia na
ni siri ya Muumba.
Makanisa mengi nchini Tanzania yana sera tofauti lakini yanaongozwa
na Biblia moja. Makanisa hayo ni Romani Katoliki, Lutheran (KKKT),
Anglikana na makanisa ya kiroho kama Full Gospel& Bible Fellowship
la Zakaria Kakobe.
FREEMASON WABARIKI
Jamii ya Freemason tayari imebariki mwisho wa dunia kwamba umefika na dunia inatarajie tukio kubwa la pamoja.
Mitandao
ya jamii hiyo inataja kama hizi ni nyakati za mavuno kwa maana kwamba,
upande wa Mungu na shetani kushindania watu huku waendao upotevuni
wakiwa wengi.
MFUMO WA DUNIA TANGU KUUMBWA
Kwa mujibu wa
kitabu kinachoitwa Panorama ya Biblia, ulimwengu tangu kuumbwa kwake
umekuwa na matukio makubwa kila baada ya miaka 2000 (inaweza isitimie au
ikapita kidogo).
Tangu kuumbwa kwa Adamu na Eva mpaka gharika inadaiwa ni miaka 2000.
Gharika hadi dunia kubadili mfumo wa mawasiliano (Mnara wa Babeli) ni
miaka 2000. Kuzaliwa kwa Yesu hadi saa ni miaka 2000 ambapo katika karne
hii, dunia huenda ikaingia katika tukio kubwa sana ambalo halijawahi
kutokea.
No comments:
Post a Comment