01 April 2015

HATIMAYE LULU MICHAEL AONYESHA MIMBA YAKE MTANDAONI

Staa mrembo kutoka Bongo Movies, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewacha njia panda  mashabiki na wafuasi wake kwenye mtandao wa INSTAGARM baada ya hapo jana usiku kubadika picha ya mwanamke mwenye ujauto na kuandika maneno ambayo hayaelezi wazi kuwa ni yeye.

“Happy New Month Lovies….Si ruksa kuitana wala ku munch”-Lulu aliandika.

Kitendo cha Lulu kuchimba mkwala akiwata watu wasiitane  kuja kuona wala kufanya kijiwe cha  kujadiliana juu ya picha hiyo (Kama inavyoonekana hapo juu) ndio kuliamsha hisia yz watu kuwa inawezekana mrembo huyo atakuwa anaujauzito hata kama picha hiyo siyo yake na hiyo anajaribu kudokeza watu kiana.

Lakini pia wapo waliochukulia ni utani tu, huku wengine wakimpongeza kwa kujaaliwa kupata ujauzito.

Lulu hakuibuka kujibu komenti nying za watu ambao zilikuwa zikihoji kana ni kweli au la.

Muda utazungumza, tuvute subra...

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname