Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amemzuia mama kijacho wake, Zarinah
Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kwenda kujifungulia nje ya Bongo pindi mambo
yatakapokuwa tayari.
Habari zilizonyakwa na Ijumaa Wikienda kutoka kwenye chanzo cha ndani ya
familia ya Diamond zilieleza kwamba, tayari jamaa huyo amemuanzishia
Zari kliniki Bongo.
“Yaani Diamond hataki kabisa Zari kwenda kujifungulia South Africa
(Sauzi). Anataka kila kitu kifanyike hapahapa Bongo. Tayari
amemuanzishia kliniki kwenye Hospitali ya AMI (ipo Masaki, Dar),” kilitonya chanzo hicho.
Akizungumzia ishu hiyo, Diamond alisema kuwa anatamani kuwa karibu na
mama kijacho wake huyo hivyo ni kweli anataka mwanadada huyo ajifungulie
Bongo.
Diamond au Baba Kijacho alisema lengo la kufanya hivyo ni ili iwe
shangwe kwa familia nzima tofauti na atakapojifungulia nje ambapo
familia italazimika kusafiri kwenda kumuona Chibu Junior.
Kwa mujibu wa Diamond, Zari ambaye ni mama wa watoto watatu akifukuzia
huyo wa nne anatarajia kujifungua kati ya mwezi Julai au Agosti, mwaka
huu.
-GPL
No comments:
Post a Comment