Msanii wa Bongo Fleva,Khadija Shabani’Keisha’ amenusurika kifo baada ya kupata ajali maeneo ya Maktaba, Posta jijini Dar.
Akizungumza na Clouds Fm alisema kuwa alikuwa akitoka chuoni CBE na
kwamba alikuwa akimfuata mumewe alipofika maeneo hayo ndipo lilipotokea
gari na kumuovateki na kuligonga gari lake. Aidha alisema kuwa alisikia
maumivu na alipokwenda hospitali kufanyiwa vipimo vilionyesha hakupata
majeraha kwa ndani.
“Nashukuru Mungu nilipimwa hospitali
vipimo vilionyesha sikupata madhara yoyote kwa ndani kwani nilikuwa na
wasiwasi labda niliumia kwa ndani,” alisema Keisha.Pole sana dada yetu. Mungu akupe afya njema!
No comments:
Post a Comment