27 February 2015

Rashidi Makwilo ‘Chid Benz’ leo ameachiliwa huru kwa kulipa faini ya Sh. 900,000

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki Rashid Makwilo 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya sh. 900,000 kufuatia kukamatwa akiwa na madawa ya kulevya.
Chid Benz (mwenye shati jeupe) baada ya kuachiwa na mahakama

Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa ya kulevya, ikiwemo misokoto ya bangi.

Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.

CHIDI BENZ HURU:Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imemwachia mwanamuziki 'Chid Benz' baada ya kulipa faini ya 900,000/= kwa kukutwa na madawa ya kulevya.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname