26 February 2015

Mzee wa Swaga: Zamaradi Amuumbua JB Kwaku-Copy na Ku-Paste!!


Mzee wa Swaga: Zamaradi Amuumbua JB Kwaku-Copy na Ku-Paste!!
Mwigizaji na mwongozaji wa filamu mkubwa hapa Bongo, Jacob Stephen ‘JB’  hivi juzi kati amekumbana na kashfa nzito ya kugeza moja ya filamu ya kutoka India ‘Bollywood’.
Filamu ya JB inayokwenda kwa jina la Mzee wa Swaga ambayo inafanya vizuri sokon hivi sasa inadaiwa kuwa ni “Copy and Paste” ya  filamu moja maarufu kutoka Bollywood inayofahamika kwa jina la "Ladies VS Ricky Bahl".
Akizungumza kupitia kipindi cha take one, Zamaradi Mketema amethibitisha usanii huo uliofanyika na kampuni maarufu ya JERUSALEM inayomilikiwa na JB, Kuwa karibia scene zote zilizochezwa na Filamu ya "mzee wa swaga" imeiga kama ilivyo kuanzia story hadi idadi ya waigizaji wakuu kutoka kwenye filamu hiyo ya kihindi iliyotoka mwaka 2011.

Mtangazaji huyo alilaani vikali utapeli huo uliofanyika na kampuni ya Jerusalem, huku JB akijifanya yeye ndiye mtunzi na mwandishi wa story hiyo wakati ukweli anaujua mwenyewe.
Bongomovies.com ilijaribu kumtafuta JB  bila mafanikio ilikuzungumzia swala hili.
Kama wewe umeziona zote hizi mbili  yani "Ladies VS Ricky Bahl" na "Mzee wa Swaga" hebu tujuze hapa

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname