Mwasiti
Almas amezungumzia salamu ya pongezi aliyopewa na Diamond Platnumz jana
kwenye siku yake ya kuzaliwa iliyovumbua uhusiano usiojulikana kati
yake na mtangazaji wa Power Jams ya EA Radio, Sam Misago.
Katika salamu hizo, Diamond aliandika: Happy Birthday Chitty… muke halali ya @Sammisago.”
Hata hivyo Mwasiti amekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Misago.
“Diamond mbona ameniweza,” Mwasiti ameiambia Bongo5.
“Sikushangaa yeye kuniwish lakini nimeshangaa response ya watu. In
short mimi sijaolewa. Yule (Misago) sio boyfriend wangu, mimi yule ni
rafiki yangu, hakuna kitu chochote kinachoendelea. Sam mimi namjua muda
mrefu sana, sijawahi kusema mahusiano yangu yoyote lakini nikiolewa
nitasema,” ameongeza.
“Sijui
Nasib kayatoa wapi haya mambo. Sam sio mwanaume wa kukupa aibu yupo
kama wanaume wengine, yule na mimi naamini ana girlfriend wake na mimi
na boyfriend wangu, kwahiyo sielewi Nasib kwakweli yaani hili suala
limeleta mtikisiko. Nimepigiwa na watu wengi sana. Lakini ukweli ni kuna
vitu havifichiki ukivifanya lazima watu watajua tu.”
No comments:
Post a Comment