Moja kati ya vyakula vinavyomletea mlaji wake harufu kali ni vitunguu swaumu ambavyo huumika kama viungo kwenye chakula .
Vitunguu swaumu vina vitu
Fulani ndani yake amvayo hujitokeza pale kinapokatwa , kusagwa au hata
kutafunwa vitu hivi kitaalamu hufahamika kama Allicin na Allin na hivi
ndio hasa husababisha harufu kali ambayo hutokea baada ya mtu kula
vitunguu swaumu au vyakula vilivyoungwa kutumia vitunguu swaumu .
Vitunguu swaumu pamoja na faida zake ka afya ya binadamu husababisha harufu mbaya mwilini.
Pamoja na hayo vitunguu
swaumu vina faida kubwa sana mwili mwa mwanadamu na faida hizo huletwa
na hii Illin ambayo inatajwa kuwa sababu ya harufu yake mbaya na moja
kati ya faida zake ni jinsi ambavyo vitunguu swaumu husaidia kupambana
na bacteria wanaoleta magonnjwa mbalimbali na virusi tofauti .
Mbegu ya Binzari
Mbegu ya Binzari hutumika
kwenye mapishi ambapo huleta ladha nzuri kwenye chakula , hata hivo
mbegu hizi husababisha harufu mbaya ambayo inabakia mdomoni kwa muda
mrefu . Kama unataka kupunguza harufu mbaya unaweza kuipunguza kwa
kunywa maji mengi na kutumia vyakula vingine ambavyo vinatumika
kupunguza harufu ambavyo havina harufu kali .
Nyama nyekundu ni moja kati
ya vcyakula vinavyosababisha harufu mbaya mdomoni na tumboni . Ni
vigumu kwa wtau wengi kukubaliana na hili kwa kua nyama nyekundu ni moja
kati ya vyakula vinavyopendwa sana na watu . Tafiti zinaonyesha kuwa
jasho jingi ambalo husababishwa na mafuta yanayoganda mwilini kutokana
na ulaji wa nyama nyekundu ni moja kati ya vitu ambavyo huleta harufu
mbaya kwenye mwili wa mwanadamu .
Nyama nyekundu ni moja kati ya vyakula sugu kwa kusababisha harufu mbaya mdomoni na inayotokea tumboni .
Kama unataka kupunguza
harufu kutokana na nyama nyekundu ni vyema ukapunguza na kuanza kula
nyama itokanayo na samaki na wanyama wengine wa baharini .
Mboga Za Majani
Baadhi ya mboga za majani zinasababisha harufu mbaya mwilini nazo ni cauliflower , kabichi, broccoli na nyinginezo nyingi .
Kahawa
Kahawa nayo iko kwenye
orodha ya vyakula ambavyo vinasababisha harufu mbaya mdomoni na mwilini
kwa jumla . Moja vitu ambavyo vimo ndani ya kahawa ambavyo ni Caffeine
husisimua mfumo wa neva yaani ile mishipa ya fahamu mwilini na
husababisha mtu avuje jasho kwa wingi kuliko kawaida .
No comments:
Post a Comment