Staa
wa muziki wa kizazi kipya, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameapa kumsaidia
mwanamuziki mwenzake David Jacob ‘Daz Baba’ anayedaiwa kujihusisha na
utumiaji wa madawa ya kulevya.
Chanzo
cha kuaminika kimeeleza kuwa, Ray C amekuwa akiumizwa na hali aliyonayo
Daz Baba na amefanya kila awezavyo hadi kuongea naye ili aanze kutumia
dozi ya Methadone ambayo wengi huipata katika Hospitali ya Mwananyamala
jijini Dar.
“Ni kweli hali ya Daz Baba inasikitisha na Ray C huyuhuyu unayemjua kaongea naye na amemshawishi kuanza kutumia dozi,” kilidai chanzo hicho ambacho ni rafiki wa Ray C.
Baada
ya kuzipata taarifa hizo, mwandishi wetu alimtafuta Ray C,
alipopatikana alikiri kuanza mazungumzo na Daz ila akaomba asizungumzie
walipofikia kwa sasa.
|
No comments:
Post a Comment