Aliyekuwa meneja wa baa ya Vijana Social ya mjini Morogoro.
ALIYEKUWA meneja
wa baa ya Vijana Social ya mjini Morogoro iliyokuwa ikimilikiwa na
Bondia Francis Cheka, Bahati Kabanda aliyemponza hadi kuhukumiwa
kifungo, hivi sasa anaishi kwa hofu kutoka kwa mashabiki wa bingwa huyo
wa masumbwi wa dunia.
Cheka alikutwa na hatia ya kumpiga ngumi na kumuumiza meneja wake huyo,
wakati alipokwenda kwa ajili ya kufuata fedha za mauzo ya baa yake hiyo
lakini wakapishana maneno yaliyosababisha tukio hilo lililowashtua watu
wengi.
Licha ya mashabiki wa bondia huyo aliyemaliza enzi za Snake Boy, Rashid
Matumla, watu wengine wanaodaiwa kumpa hofu Baraka ni pamoja na
wakusanya chupa za plastiki ambao walimtegemea Cheka kwa ajili ya kwenda
kuziuza katika kiwanda chake kilichopo maeneo ya Kihonda mjini hapa.
“Ukweli
maisha ya huyu jamaa hapa Morogoro ni magumu sana kwa sababu kila
anakokwenda anakutana na watu wanaomnanga juu ya kitendo alichokifanya.
Watu wanaomtakia mema wanamshauri kuwa mwangalifu sana wa nyendo zake
kwani watu wanaweza kumfanya lolote maana Cheka ni mtu muhimu sana
hapa,” alisema shuhuda mmoja
No comments:
Post a Comment