Vanessa Mdee ni balozi wa makampuni makubwa mawili nchini Tanzania.
Akiongea nasi hivi karibuni, Vanessa alidai kuwa inahitaji qualities kadhaa kwa msanii kuweza kupewa kazi hiyo.
“Kikubwa sana ni msanii ni kujithamini na kujitambua kama a brand
yeye mwenyewe kama msanii au mtu ambaye unafanya sanaa. Uwe muigizaji,
muimbaji yeyote yule,” alisema Vanessa.
“Bidhaa zipo nyingi sana duniani. Naamini kuwa kila msanii ambaye
atajirepresent kama brand atapata bidhaa ambayo ingependa kuambata naye
kwasababu wamefanana. Kwahiyo tafuta kitu ambacho ni special kwako. Ni
vitu vya kuzingatia kujitambua na kujifahamu kama brand na kitu gani
unachokiweza zaidi.”
“Naamini kwa kufanya hivyo itawafungulia wasanii wengi milango mingine ya kufanya endorsement ni muhimu sana kwa msanii,” alisisitiza.
No comments:
Post a Comment