Diamond Platnumz ni miongoni mwa marafiki wa karibu wa msanii Dully
Sykes ambaye weekend iliyopita alimpoteza baba yake mzazi Ebby Sykes,
lakini hakuweza kuhudhuria msiba huo kutokana na sababu ambazo amezitoa
leo.
Diamond ambaye wakati msiba huo unatokea alikuwa Zanzibar na mpenzi wake
Zari, ameelezea sababu zilizomfanya kushindwa kuhudhuria mazishi.
“Watu waliniona niko zanzibar lakini walikuwa hawajui nimeenda
kufanya nini,” Diamond ameiambia 255 ya XXL ya Clouds FM. “Usiangalie
kila unachokiona Instagram ukajua mtu labda kwasababu alikuwa anafanya
starehe. Niko katika kipindi ambacho sio kizuri kwangu mimi na familia
yangu kwasababu kuna vitu ambavyo siwezi kuvizungumza lakini, na siwezi
kuviweka kwenye media ndo maana watu wengine wanaweza kuniona nacheka
lakini […] kwanza mama yangu anaumwa na anaumwa sana sijawahi
kulizungumza hili ndo nalizungumza hapa, hapa ninapoongea na wewe yupo
India, kuna vitu vingi vinaendelea, siwezi kusema nilikuwa Zanzibar
nafanya nini, inawezekana ikawa ndo sababu iliyonifanya mpaka mimi
nikachelewa kwenda kwenye msiba, lakini inawezekana labda mimi ndio
nilikuwa mtu wa kwanza kutoa pole katika social networks zangu mimi.”
“Unajua wakati mwingine ni vizuri kwenda kuzika lakini inawezekana
mtu akawa ameenda kuzika lakini mi nikawa sijaenda kuzika nikawa
nimefanya kitu cha maana kuliko wale walioenda kuzika kwasababu huwezi
kujua nilifanya kitu gani. Nilisikia niliambiwa watu walikuwa wanongea
sijui Diamond hajafika lakini naamini kuna watu wengi hawakufika na kila
mtu hakufika kwa sababu fulani. Dully mi ni kama kaka yangu kabisa ni
mtu ambaye amenisaidia vitu vingi sana isingewezekana kabisa niko
ninanafasi nishindwe kwenda kwenye msiba.”
“Ukiacha tu Dully mwenyewe kwanza mtu aliyefariki ni kama mzee wangu,
na mtu ambaye amefanya kitu kikubwa katika sanaa hii ya muziki na mimi
nimefika hapa yeye pia ana mchango wake, so haikuwa rahisi eti mimi
nisiende tu nikiwa sina sababu, kulikuwa na sababu na ndio maana.” Alimaliza Diamond
No comments:
Post a Comment