
Mkali katika tasnia ya filamu Bongo, Aunt Ezekiel. Akizungumza na
gazeti hili hivi karibuni jijini Dar, Aunt alifunguka kwamba, mbali na
kumzushia juu ya ujauzito huo, kuwa mara ya kwanza watu asiowajua
walieneza uvumi kuwa alikwenda nchini Marekani na mheshimiwa huyo lakini
aliwapuuza kwa kuwa alikwenda kwa kazi yake ya sanaa.
“Kuna binadamu hawajali maumivu ya mtu mwingine, inawezekanaje mtu
aanze kuropoka kitu kizito kama hicho tena mtu na familia yake, sasa mtu
ambaye ndiye muhusika wa ujauzito huu anajisikiaje?“Ukweli mimba yangu
siyo ya waziri, ifahamike kuwa namheshimu sana mheshimiwa, najisikia
vibaya mtu anapoeneza kitu cha namna hiyo,” alisema Aunt kwa uchungu
mkubwa.
Aunt alitiririka kwamba, mbali na uvumi huo, pia alishangazwa na
baadhi ya wabunge waliothubutu kuzungumza kuhusu yeye na waziri huyo
tena bungeni kwenye kujadili vitu vya msingi badala yake wanazungumza
mambo ambayo hayana kichwa wala miguu.
“Hivi inawezekana kweli kabisa wabunge ambao tunawaheshimu wanakwenda kuzungumza vitu vya ajabu bungeni?
Akiwa katika pozi. “Wamenifanya nisiwe naangalia hata hilo bunge kabisa,” alisema Aunt.
Staa huyo alimalizia kuwa mambo hayo yanampa wakati mgumu na
kumuumiza kwa sababu madai yanayozungumzwa ni mazito huku yakiwa hayana
chembe ya ukweli zaidi ya kuleta mfarakano kwenye familia ya waziri huyo
ambaye pia ni mbunge.
Mbali na waziri huyo, pia Aunt alikanusha kuwa mimba kubwa aliyonayo
si ya yule mcheza shoo wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’, Mose Iyobo
kama wengi wanavyodai.
Kuhusu hilo, gazeti hili lilizungumza na Mose Iyobo ambaye alisema
kuwa anachojua ujauzito ni wa kwake lakini akashangazwa na uzushi
usiokuwa na kichwa wala miguu.
Akiwa na shoga yake Wema Sepetu. Baadhi ya mashabiki wa Aunt
waliozungumza na gazeti hili walionesha kubaki na alama ya ulizo kwamba
kama Aunt anamruka Mose Iyobo na amekasirishwa na tetesi za kuhusishwa
na waziri huyo ambaye ni mume wa mtu huku mumewe, Sunday Demonte
akidaiwa kufungwa Dubai, je, mimba hiyo ni ya nan
No comments:
Post a Comment