06 February 2015

ALIYEMUAWA YULE ASKARI WA DODOMA AKAMATWA AKIWA NA LILE PANGA ALILOMUUWA NALO ASKARI...WANANCHI WAMSHAMBULIA KWA HASIRA


Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa alinaswa majira ya saa 23:00hrs usiku wananchi walimuona maeneo ya Mti Mkavu Mailimbili Mkoani Dodoma akiwa bado na lile panga alilotumia kumuua Askari.

Hata hivyo walichukua sheria mkononi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake, Polisi walifika eneo la tukio na kumchukua kisha kumkimbiza Hospitali ya Mkoa lakini daktari akagundua ameshafariki.

Aidha Kamanda MISIME amesema mtuhumiwa huyo katika kumbukumbu tulizonazo ni kwamba mwaka 2006 aliwahi kufungwa miaka mitatu (3) kwa kosa la kujeruhi, Pia mwaka 2009 alifungwa tena miezi sita (6) kwa kosa la kutishia kuua.

Ametoa pongezi kwa wananchi kwa kuonyesha kuchukizwa na kitendo alichomtendea Askari wetu lakini waache kujichukulia sheria mkononi. Pia ametoa wito kwa wananchi tuanze kuchukua hatua kurekebisha maadili kuanzia ngazi ya familia kwani tumeelezwa kuwa mtuhumiwa alikuwa ni mvutaji bangi kiasi kwamba ilimfanya awe anafanya vitendo ambavyo ni kinyume na maadili na sheria za nchi

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname