Unyama! Dada wa kazi (hausigeli), aliyetajwa kwa jina moja la Rachel, mkazi wa Tabata-Shule jijini Dar, anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kuchukua kisu jikoni kisha kumchomachoma nacho mtoto, Samwel John (4) anayeishi nyumba ya jirani.
John alisema kwamba, hausigeli huyo alimwambia kuwa mtoto alikuwa amegongwa na pikipiki lakini mtoto alikataa huku akimnyooshea kidole yule dada wa kazi.
Mzazi huyo aliendelea kusema kwamba, baada ya kuona hivyo alimshika mkono mwanaye hadi kwenye nyumba ambayo anafanya kazi msichana huyo huku mtoto huyo akimuongoza chooni ambapo alikuta damu nyingi zimetapakaa.
Alisema kuwa alipoona hivyo ilibidi amchukue mwanaye na msichana huyo hadi polisi kwa ajili ya kupata PF-3 kwa ajili ya matibabu.Kwa upande wake hausigeli alipoulizwa ni kwa nini alifanya kitendo cha kinyama kiasi hicho alisema kuwa alikuwa akitamani kumtoa jicho mtoto huyo.
Baada ya kujieleza, hausigeli huyo alitupwa korokoroni nyuma ya nondo za mahabusu kwa kitendo alichokifanya ambapo hadi gazeti hili linaanua jamvi maeneo hayo alikuwa kwenye Kituo cha Polisi cha Tabata akisubiri sheria ichukue mkondo wake.
No comments:
Post a Comment