Kituo
cha redio cha Times FM na kampuni ya Times Promotions, wamewasilisha
mashtaka mahakamani ya kutaka viongozi wa juu wa Clouds FM pamoja na
msanii wa Nigeria, Davido wapelekwe jela kwa kukaidi amri ya mahakama.
Kampuni hiyo kupitia wakili wake Peter Kibatala imewasilisha mashtaka hayo katika mahakama ya
hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Jumatatu hii.
hakimu mkazi ya Kisutu jijini Dar es Salaam Jumatatu hii.
Katika
kesi hiyo, inadaiwa kuwa Davido na Clouds FM walikaidi amri ya mahakama
iliyotolewa kumtaka Davido asitumbuize kwenye tamasha la Fiesta
lililofanyika October 18 kwenye viwanja vya Leaders jijini Dar es
Salaam.
Times
FM walikuwa wameshaingia mkataba na Davido atumbuize November 1 kwenye
tamasha lao ambalo linadaiwa kuahirishwa kutokana na kilichotokea.
Soma zaidi habari hiyo iliyoandikwa kwenye gazeti la leo la Daily News hapa.
No comments:
Post a Comment