06 October 2014

KIJANA AGONGWA NA GARI MBEYA KISHA KUFARIKI PAPO HAPO

Mtembea kwa miguu aliyefahamika kwa jina la Robert Mgala (21) mkazi wa Ihanda alifariki dunia baada ya kugongwa na gari isiyofahamika namba zake za usajili lililokuwa likiendeshwa na dereva asiyefahamika jina wala makazi yake. 
Ajali hiyo imetokea mnamo jana majira ya saa 16:00 jioni huko katika kijiji cha Ihanda, kata ya Ihanda, tarafa ya Vwawa, wilaya ya Mbozi, mkoa wa Mbeya
katika barabara ya Mbeya/Tunduma. Chanzo cha ajali kinachunguzwa. Dereva alikimbia mara baada ya ajali hiyo, jitihada za kumtafuta zinaendelea. 
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Mbozi. SOMA ZAIDI>>>

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname