28 October 2014

HATARI: BILIONEA WA UNGA ATIKISA DAR! MKASA MZIMA UPO HAPA!

Mfanyabiashara bilionea jijini Dar, Mharami Mohamed Abadallah ‘Chonji’ ((mwenye suti ), akiwa chini ya ulinzi. Mtikisiko huo umekuja kufuatia maeneo mbalimbali ya jiji kumzungumzia kwa namna mbili, wengine wakifurahia wengine wakisikitika, hasa wanawake wanaoishi maeneo ya Magomeni Kondoa, Dar ambako mfanyabiashara huyo ndiko kwenye makazi yake. 

HII kali! Kukamatwa na polisi kwa mfanyabiashara bilionea jijini Dar, Mharami Mohamed Abadallah ‘Chonji’ (44) (aliyezungushiwa duara) hivi karibuni akidaiwa kukutwa na madawa ya kulevya ‘unga’ aina ya heroin yenye thamani ya shilingi 300,000,000 kumelitikisa Jiji la Dar, Uwazi limefuatalia hatua kwa hatua.
 
AKUTWA NA SARE ZA JESHI
Tukio lingine liliwatikisa polisi wenyewe kufuatia upekuzi wa kina nyumbani kwake ambapo walimkuta pia na sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zinazofanana kwa sehemu kubwa na zile zilizomwingiza Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwenye mzozo na jeshi hilo.

Sare mpya za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) zilizokamatwa nyumbani kwa Billionea huyo.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname