Mpiga picha na graphic designer anayefanya kazi kwenye kampuni ya I-View Studios, ni mwakilishi wa kwanza kutoka Tanzania aliyetajwa tayari kutuwakilisha mwaka huu kwenye shindano la Big Brother Africa. Majina bado yanaendelea kutajwa hivyo tunangoja kufahamu mshiriki wa pili.
Tumepata bahati ya kukutana na Idris. Ni kijana mwenye vituko sana na
ukikaa naye kwa muda mfupi lazima akuvunje mbavu kwa maneno yake ya
papo kwa papo ambayo yatakufanya ugundue kuwa ucheshi ni kitu
alichobarikiwa na mwenyezi Mungu.
Kwa wajihi wake, Idris ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye jumba hilo litakalozinduliwa rasmi Ocotber 5.
No comments:
Post a Comment