Serengeti
Fiesta September 7 2014 Musoma, show ambayo ilifanywa maalum baada ya
maamuzi kufikiwa ili upendo usambazwe kwa wote waliofiwa na
waliojeruhiwa kwenye ajali ya Mabasi iliyoua 39 Musoma September 5
2014.Show ilikua ifanyike Ijumaa lakini iliahirishwa siku hiyohiyo baada
ya ajali kutokea na ilikua isifanyike moja kwa moja, Jumamosi watu
ikiwa ni pamoja na Wasanii wakiwa wamejiandaa na safari, stage kianza
kuondolewa ili kusafirishwa…. likaja wazo kwamba inaweza kufanyika show
ya Fiesta lakini ikawa maalum kwa ajili ya ajali ya
Ijumaa.Matangazo yalianza kuruka Jumamosi jioni na Jumapili ambapo
kiukweli hatuna budi kuwashukuru watu wote waliojitokeza kutoka hata nje
ya Musoma na kuja kwenye Fiesta Jumapili hii iliyofanyiwa kazi na
Christian Bella, Nay wa Mitego, Chege na Temba, Stamina, Nikki wa II,
Young Killer, Shilole, Recho, Roma Mkatoliki na wengine waliokubali
malipo yao yakatwe na yapelekwe tena kutoa msaada kwa mara ya tatu
hospitali siku ya Jumatatu.
Wasanii
waliwasha mishumaa mwishoni mwa show na wote wakapanda kwenye stage kama
ishara ya kuwakumbuka wote 39 waliopoteza maisha kwenye ajali ya Ijumaa
Musoma.
Dj Fetty
aliwaongoza wakazi wa Musoma kuimba single ya ‘Kamanda’ wakati wa
kuwakumbuka wote waliofariki kwenye ajali ya Ijumaa Musoma.
No comments:
Post a Comment