| Rais wa Wasanii wa Bongo Muvi Steve Nyerere ametangaza kujizuuzulu rasmi nafasi yake hiyo kuanzia sasa hivi na
kwamba kesho asubuhi atazungumza na Waandishi wa habari katika Ukumbi
wa Maelezo hapa mjini kuelezea kwa kirefu kuhusu uamuzi wake huo.
Akuzungumza na Blogu hii muda mchache uliopita Steve alikuwa akiongea
kwa upole sana na kusisistiza kwamba hatatoa maelezo leo mpaka kesho,
juhudi zote za hii blog kumbana aseme sababu ya uamuzi wake huo wa
ghafla Steve alisema ni kesho tu ndio atatoa maelezo kwa anayetaka kujua
na kusikia sababu aje kesho Asubuhi Maelezo. |
No comments:
Post a Comment