20 September 2014

MAYA WA BONGO MOVIE APATA KIGUGUMIZI NDOA YAKE

Mkongwe kwenye kilinge cha filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’.

MKONGWE kwenye kilinge cha filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’, amepata kigugumizi cha ghafla kuzungumzia ndoa yake ambayo maandalizi yake ya awali yaliwahi kufanyika.
Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kuulizwa kuhusiana na ndoa hiyo iliyokuwa ifanyike mwaka juzi, Maya alishindwa kuzungumzia jinsi ilivyoyeyuka na badala yake aling’atang’ata maneno huku akidai haelewi ilipoyeyukia.




“Kuhusu ndoa mh! yaani sijui bwana nitazungumza nini kuhusu hilo daah, sijui hata iliishiaga wapi,” alisema Maya ambaye alitaka kuolewa na ‘mzee’ mmoja hivi ambaye alikuwa akimficha jina lake.

No comments:

Post a Comment

Comments system

Disqus Shortname